Kindau (Bantu)

Kindau ni lugha ya Kibantu nchini Msumbiji na Zimbabwe inayozungumzwa na Wandau. Isichanganywe na lugha ya Kindau izungumzwayo nchini Indonesia. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kindau nchini Msumbiji imehesabiwa kuwa watu 1,580,000. Pia kuna wasemaji 800,000 nchini Zimbabwe. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kindau iko katika kundi la S10. Kindau kinafanana sana na Kishona, na wataalamu wengine wanakiangalia kama lahaja ya Kishona tu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne